Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA- , Kitabu kiitwacho: "Baba Hadi", ni kitabu cha kwanza kwa ajili ya Watoto na Vijana kuhusu maisha ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ambacho tayari kimechapishwa. Kitabu hiki kinajaribu kusimulia vipengele vya maisha ya Shahidi huyu Mkuu kwa njia ya Hadithi rahisi na nyepesi, kwa maana kimesheheni hadithi nzuri, nyepesi na rahisi, zinazoeleweka na zenye athari chanya na nzuri kwa watoto. Hakina Hadithi ambazo zinaeleweka na kufahamika kwa watoto tu, bali pia Hadithi hizo zinafahamika na kueleweka kwa watu wa rika zote na zinaweza kusaidia kutengeneza na kuunda haiba zao.
Kitabu hiki cha "Baba Hadi" kina muundo uliorekodiwa kabisa - kwa maana ni (Documentary) kamili , kwa kutumia kumbukumbu na matukio halisi kutoka katika maisha ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, na kwa mantiki hiyo Kitabu kinatoa picha ya wazi na inayoonekana ya utu wake katika akili ya mtoto na kijana. Kazi hii ilitayarishwa kwa lengo la (kuwajulisha au kuwafahamisha au) kuwatambulisha watoto kwa watu wakubwa - watu wenye shakhsia kubwa - na wenye ushawishi mkubwa. Ujuzi huu kuupata wakati wa utotoni, unaweza kuwafungulia watoto njia ya kufuata mfano bora wa takwimu hizi za shakhsia kubwa katika ujana wao, na hatimaye kufuata mtindo wao wa maisha katika utu uzima wao.
Mwandishi wa kitabu hiki amechukua uangalifu wa pekee kabisa katika kuchagua nukta maridadi kutoka kwenye maisha ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah ili kujumuisha mafundisho ya vitendo yanayoweza kutumiwa na watoto katika maisha yao ya kila siku. Nukta hizi ni pamoja na kuwaheshimu Wazazi (Baba na Mama), Kukubaliana na hali za familia, Kuwajibika, Kuwasaidia wazazi, Umuhimu wa elimu, Kuwa na mahusiano na Mwenyezi Mungu, Kuwa na ukaribu na Sala na Qur'an, na Haja ya kupiga vita dhuluma.
Jina la Kitabu hiki ambalo ni: "Baba Hadi" pia lilichaguliwa kwa kuzingatia haiba na hadhi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah. Jina hili ni tafsiri ya lakabu yake maarufu, "Abu Hadi"; Jina ambalo, kwa upande mmoja, linarejelea jukumu lake la ubaba kwa watoto wa Lebanon, kwa watoto wa Wapalestina, kwa watoto wa Syria, na kwa Watoto wa Mashahidi, na kwa upande mwingine, jina hilo linatukumbusha uhusiano wake maalum na mashuhuri kwa mwanawe aliyeuawa kishahidi, aliyeitwa: Sayyid Hadi Nasrallah.
Kitabu hiki: "Baba Hadi", kilichoundwa kwa juhudi na hima ya Jumuiya ya Watoto na Vijana wa Fikra (Chughok) na kuandikwa kwa kalamu ya Elaheh Akherati, kinaonyesha mambo ya maisha ya Sayyid Hassan Nasrallah katika mfumo wa hadithi ya watoto kikiwa kwenye kurasa 24, na bei yake ni Toman 85,000 (sawa na Shilingi elfu mbili au elfu moja na mia tano ya Tanzania / 1,500 Tshs).
Your Comment